Thursday, July 17, 2014

KWA TAARIFA YAKO: KWAYA ILIYOZINDUA KWAYA NYINGINE DAR, YATOKA KIVINGINE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu
 ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO msomaji wa GK leo ni kuhusiana na maendeleo ya kwaya zetu nchini Tanzania, ambazo kwa namna moja ama nyingine kufanya kwao vizuri kunatokana na kuona jambo zuri kutoka kwenye kwaya nyingine zilizopo nchini ama nje ya nchi, kitu ambacho ni kizuri kwakuwa kinawapa waimbaji na wapigaji wa kwaya husika kubadilika na kuongeza kitu ambacho wanadhani kimepungua kutokana na namna wenzao wanavyofanya.

KWA TAARIFA YAKO kuna suala la uzinduzi wa video na audio za kwaya mbalimbali nchini ambazo umaarufu wa kuzindua kunaendana na mgeni wa heshima ambaye atachangia kiasi cha fedha ili kuiwezesha kwaya husika kusonga mbele katika mipango ya injili waliyojiwekea. Mwanzoni uzinduzi haukuwa maarufu nchini, kwaya ama waimbaji binafsi walikuwa wakibariki kazi zao makanisani mwao bila matangazo ya kwamba watakuwa na tukio hilo labda upate kusikia kutoka kwa watu wanaosali kanisa ambalo kwaya hiyo wanatoka.

KWA TAARIFA YAKO kwaya iliyofungua kwaya nyingine nchini hususani kwa jijini Dar es salaam kufanya mambo ya uzinduzi na matangazo kuonekana kwenye runinga ni kwaya ya 'Neema
N.G.C wakati wa uzinduzi album mpya hivi karibuni.
Gospel Kwaya' kutoka kanisa la African Inland Church (AIC). Kwaya hii ilizindua video yake ya kwanza iitwayo 'Dunia Imechafuka' mwanzoni mwa miaka ya 2000 na matangazo ya uzinduzi kurushwa kwenye runinga ya ITV (kama GK haijakosea) huku ukumbi ukiwa Diamond Jubilee VIP. Haikuwa ajabu kwa video kwakuwa kwaya kama Ulyankulu Tabora, Tumaini Shangilieni Kwaya Arusha,  na Uinjilisti Sayuni Kinondoni Lutheran walikuwa wameshatoa video zao miaka mwishoni mwa miaka ya 90.

KWA TAARIFA YAKO ninachotaka ukifahamu ni kwamba Neema Gospel Choir (N.G.C) ndio kwaya ya kwanza kufanya uzinduzi mkubwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kutangaza uzinduzi wao kupitia runinga. Baada ya Neema kufanya uzinduzi wao uliofanikiwa sana, kwaya nyingine zikafuata kwa kuanza kutangaza zinduzi zao pamoja na kukodi kumbi za kuzindulia wakati awali ilikuwa wanazindulia makanisani mwao.




KWA TAARIFA YAKO kama haitoshi baada ya kutoa kanda hiyo ya 'Dunia Imechafuka' Neema wakaendelea na huduma na kufanikiwa kutoa video nyingine huku pia ikishuhudiwa kwaya kama Haleluya kutoka Tabata wakitangaza kanda yao 'Unang'ang'ania dhambi itakupeleka pabaya' ikipata umaarufu kwa kuonyeshwa kwenye runinga pamoja na kwaya nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanya uzinduzi. KWA TAARIFA YAKO kama haitoshi Neema iliongeza nguvu kwenye masuala ya muziki miaka takribani sita sasa kwakupata timu ya vijana wanaopiga muziki mzuri kama ilivyoshuhudiwa kwenye video yao ya 'Kuna mamba Kivukoni'. Sasa ni takribani wiki mbili toka kwaya hiyo izindue album yake mpya ya sauti iitwayo 'Haki yake Mungu' moja kati ya album bora za muziki wa injili nchini kwa ujumla. 

KWA TAARIFA YAKO miaka mitatu iliyopita kulikuwa na picha ya sauti (video) ya kundi la Joyous Celebration ya Afrika ya kusini (Joyous 15 part 1) ambayo iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook na mmoja wa wanamuziki wa kwaya hiyo na majadiliano yakaanzia hapo, katika majadiliano hayo wanamuziki hao wakasema inawezekana kabisa kwaya ikapiga viwango vya Joyous hata kuzidi kama watu wataamua kuwa serious, maneno hayo ndiyo nayaona majibu sasa, mwanzo wa sasa wa Neema Gospel ni kweli inataka kuimba viwango vya juu zaidi na kutaka kufahamika kimataifa, ili kujua nazungumzia kitu gani nunua album yao mpya utaamini kwanini nimekujuza.


Timu ya wanamuziki Neema Gospel Choir.

No comments:

Post a Comment