Friday, July 18, 2014

mwanza chior

mfuko wa pensheni wa pspf

ONSPOT MAGAZINE

ONSPOT MAGAZINE
Home » » MWANANCHI GOSPEL SINGERS KUTOKA MWANZA WAZINDUA ALBAMU YAO YA VIDEO KWA KISHINDO.

MWANANCHI GOSPEL SINGERS KUTOKA MWANZA WAZINDUA ALBAMU YAO YA VIDEO KWA KISHINDO.


Kwaya ya Mwananchi Gospel Singers kutoka Mwanza wakiimba kwa umakini katika uzinduzi wa albamu yao ya Roho Yaumia katika kanisa la Aic Nyakato Mwanza jana.
                                                  Wakiwajibika stejini.
                                                             Utawapenda ile mbayaa.
           Hapa wanaonyesha moja kati ya staili zao ambazo ziliwabariki watu wote katika viwanja hivyo.
                                              Kwaya ya Aic Nyakato wakiwa stejini.
                                                    Kwaya ya Aic Nuru Butimba
                                                      Kwaya ya Aic Vijana kutoka Nyakato.
                                                     Kwaya ya CGM kutoka mahina.
                                                     Kwaya ya Neema Aic Nyakato.
                                  Kwaya ya Aic Igoma nao wakiwa stejini kama kawaida yao.
                                          Kwaya ya Nyakato Moravian kutoka Nyakato.
                   Wageni waalikwa Mr John Mtemi na Mwalimu John Kutoka eagt Buzuruga Mwanza.
Watoto nao hawakuwa nyuma kujitokeza katika kuwaona waimbaji mbalimbali wakiimba kwa Mungu baba.
                                Wageni Waalikwa kwa hafla ya Uzinduzi wa Albam.
                                                      Nyomi ndani wa Uwanja.

USIKOSE JUMAPILI HII NDANI YA VIWANJA VYA AIC CHANG'OMBE!!!!!!!

HABARI NJEMA NDANI YA AIC CHANG'OMBE JUMAPILI HII



Kwaya ya Neema Gospel live kutoka kanisa la AIC Chang'ombe jijini Dar es salaam wanatarajia kufanya ibada kubwa ya kusifu na kuabudu jumapili hii kanisani kwao ikiwa maalumu kwaajili ya kuachia video ya wimbo wao "Ponya Kanisa lako" maalumu waliourekodi kwaajili ya kuombea kanisa la Tanzania.

Kwa mujibu wa katibu wa kwaya hiyo kijana Samuel John Nkola amesema wanategemea kuona Mungu akikutana na haja za watu wake hasa kutokana na maandalizi mazuri yanayofanywa na kwaya hiyo katika suala zima la maombi pamoja na mazoezi ya uimbaji ambayo wamesema mpaka sasa hawana wasiwasi na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kufika bila kukosa kuanzia majira ya saa 8 mchana na kuendelea, ambapo watasindikizwa na wenzao wa Chang'ombe vijana Choir(CVC) ama waite wana wa Vunja, Matendo kwaya na waimbaji wengine na kwamba itakuwa hakuna kiingilio.

Samuel amesema kwa watu watakaofika siku ya jumapili watafaidika kwakuondoka na video ya wimbo huo ambao audio yake imesambaa katika mitandao na radio mbalimbali. Kwaya hiyo ambayo kwasasa imekuwa ikiacha gumzo kwa uimbaji na upigaji wao maridadi kila sehemu wanakoalikwa, wanatarajia kufanya live DVD rekodi mapema mwezi wa pili mwakani huku kanda ya sauti ya nyimbo wanazotarajia kurekodi wanatarajia kuiachia mapema mwezi wa kumi mwaka huu.Usikose Chang'ombe sokota jumapili hii kiingilio bure.

UJIO WA ALBAM MPYA KUTOKA KWA MWANA DADA ROSE MHANDO

Kamata Pindo la Yesu

MZEE WA UPAKO AKIELEZEA JINSI ALIVYO KAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

MZEE WA UPAKO:NILIKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA

LITOKEA lakini haikuandikwa kwa sababu haikudakwa! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi jijini Dar es Salaam (GRC), Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kuwa aliwahi kukamatwa na kuwekwa lupango katika Gereza la Keko, Dar kwa siku 14 akituhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ‘unga’, Risasi Jumamosi lina sauti yake.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’.
Akizungumza kwa uso wenye majonzi na siha ya huzuni mwishoni mwa wiki iliyopita kanisani kwake Ubungo- Kibangu, Dar, Mzee wa Upako alisema hawezi kuisahau siku hiyo ambayo shetani aliamua kukunjua kucha zake kumwelekea yeye.
Alisema ishu hiyo ilimkuta mwaka 2005 akiwa tayari mtumishi wa Mungu aliye hai, lakini anachomshukuru Mungu ni kwamba alimsimamia kwa nguvu zote.

MCHEZO MZIMA ULIVYOKUWA
Akizungumzia mchezo mzima ulivyokuwa, Mzee wa Upako alisema siku ya tukio (hakuitaja) akiwa kanisani hapo na waumini wake ghafla walitokea askari polisi ambao idadi yao haikumbuki.
Alipotaka kujua shida yao, walisema wao wanatokea Polisi Central, Dar na walikwenda pale kufanya naye mahojiano na kumpekua kwani alikuwa akihisiwa anajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.“Polisi walikuja kanisani wakafanya upekuzi, wakaenda nyumbani  nako wakafanya hivyohivyo kisha wakaondoka zao baada ya kutokuona chochote,” alisema Mzee wa Upako.
                                                                               Kamanda Nzowa.

POLISI WA INTERPOL WATUMIKA
Mzee wa Upako anaendelea kufunguka: Siku mbili mbele  wakaja wengine, wakasema wao ni Polisi wa Kimataifa (Interpol). Nao wakasema wamekuja kunipekua, lakini wao licha ya kutokukuta chochote walinikamata na kunipeleka Mahabusu ya Gereza la Keko, Dar ambapo nilikaa kwa muda wa kama wiki mbili.

AZITAJA SIKU ZA MAJARIBU
Mzee wa Upako: Hakika zilikuwa ni siku za majaribu kwangu kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, lilikuwa ni jambo ambalo sijawahi kulifanya achilia mbali kuliwaza.
Licha ya kukaa kwa wiki mbili kule mahabusu, Polisi wa Interpol nao walijiridhisha kwamba mimi sifanyi biashara hiyo, wakaniachia huru niendelee kumtumikia Mungu wangu.
                                                                 Madawa ya kulevya.

AWAGUNDUA WABAYA WAKE
Mchungaji huyo maarufu kwa msemo wake WATASHINDANA, LAKINI HAWATASHINDA aliendelea kusema kuwa aligundua kukamatwa kwake kulitokana na mpango wa siri uliofanywa na baadhi ya wachungaji wenzake (hakuwataja majina) kwa ajili ya kumdhoofisha kiimani.
“Zilikuwa ni mbinu chafu za kunidhoofisha kiimani kutoka kwa baadhi ya wachungaji wenzangu wenye wivu na huduma yangu. Lakini kwa jina la Yesu aliye hai walishindwa, watashindana lakini hawatashinda,” alisema Mzee wa Upako.

AHISI KUONDOLEWA HADHI
Mzee wa Upako alisema tukio hilo aliliona kama la kumwondelea hadhi katika jamii, hususan kwa waumini wake lakini kwa kuwa yeye ni ‘super charge’ kamwe hawezi kuruhusu imani yake iyumbishwe na hila za muovu shetani.

ANACHOMSHUKURIA MUNGU
Mchungaji huyo alisema baada ya kutoka Keko alimshukuru Mungu kwa vile hakuna chombo chochote cha habari kilichofuatilia juu ya sakata hilo na kwamba gazeti hili (Risasi Jumamosi) linakuwa la kwanza kuandika.
“Nashukuru hakuna chombo chochote cha habari kilichogundua juu ya habari hiyo, ninyi mnakuwa wa kwanza kuijua na hata kuiandika kama mtapenda,” alisema Mzee wa Upako.

APINGA DHANA YA WATUMISHI WA MUNGU KUUZA UNGA
Akizungumzia kwa undani sakata la watumishi wa Mungu kujihusisha na biashara ya unga, Mzee wa Upako alisema:
“Siamini kama kweli kuna watumishi wa Mungu wa hapa Tanzania wanafanya biashara hiyo. Kinachotokea ni kwamba, watu wamekuwa wakiwasingizia watumishi kwa sababu zao.”

WAUMINI WAKE SASA
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi liliwasiliana na baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambapo walisema mtumishi wao huyo amekuwa akionewa kijicho kutokana na mafanikio yake ya kiroho na kimwili.
“Sisi waumini wa GRC tukisikia lolote baya kuhusu Mzee wa Upako huwa hatushtuki kwa sababu wapo baadhi ya watumishi wa Mungu wanamuonea kijicho kwa sababu ana mafaniko ya kiroho na kiimani,” alisema muumini mmoja bila kutaja jina.
Mwingine alisema nguvu kubwa ya kiroho aliyonayo mtumishi huyo imemfanya aibue maadui wasio na hofu ya Mungu kwa kumpakazia skendo mbalimbali wakiamini akichafuka waumini watamkimbia.
Jumatano iliyopita, paparazi wetu alifika Kituo Kikuu cha Polisi (Police Central), Dar na kuulizia ishu hiyo ambapo afande mmoja alisema anayeweza kujua ni IGP Mstaafu, Omary Mahita ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya kiganjani kutokupatikana hewani.
Views: 3832
Tags: risasi11
Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers
Comment by king jaja on November 10, 2013 at 9:17am
JE JESHI LA POLISI NIMECHUKULUWA ATUA GANI KUHUSU KUKAMATA NA KUWAPIGA WATU WANAOSINGIZIWA WANAUZA MADAWA?
jeshi la polisi tanzania linajua kabisa wauza madawa wa kubwa ni wabunge,mawaziri na wafanyabiashara wakubwa,
swali ni kwamba hatuoni polisi wakienda kuwakagua wabunge,bali wanakagua watu ambao wajua kabisa hawana madawa.Jeshi la polisi tanzania ni jeshi lililokosa wasomi.
Ninacho wa shauri watu wao kamatwa na kupotezewa muda:
1.mzee wa upako,alifungulie kesi jeshi la polisi kwa kumpotezea muda wake wa siku 14 gerezani/jela
2.pia afungue kesi ya kuzalilishwa na jeshi la polisi,sababu polisi wanapaswa kumkamata mtu na kumuweka ndani wakimkuta na dawa siyo kujichukulia sheria ya kumbambikizia mtu keshi.
3.pia afungue kesi ya kukosa imani na polisi ,kwani next time watamuwekea kete ili aende gerezani,hasipo ifungulia polisi kesi ,polisi itamuua yeye.

mwisho "kwanini jeshi la polisi tanzania linafanya kazi kisanii,kila wakati hawa kamati mtu/watu wahusika wanakamata mtu bandia"
WATANZANIA HATUNA IMANI NA JESHI LA POLISI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

AIC nyakato mwanza kwaya

  1. Nimeona Mateso- AIC NYAKATO CHOIR

    Mimi Ni Mtu Aliyeona Mateso. you can feel the Soloist showing It in Her face. Wonderful song.

Thursday, July 17, 2014

KWA TAARIFA YAKO: KWAYA ILIYOZINDUA KWAYA NYINGINE DAR, YATOKA KIVINGINE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu
 ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO msomaji wa GK leo ni kuhusiana na maendeleo ya kwaya zetu nchini Tanzania, ambazo kwa namna moja ama nyingine kufanya kwao vizuri kunatokana na kuona jambo zuri kutoka kwenye kwaya nyingine zilizopo nchini ama nje ya nchi, kitu ambacho ni kizuri kwakuwa kinawapa waimbaji na wapigaji wa kwaya husika kubadilika na kuongeza kitu ambacho wanadhani kimepungua kutokana na namna wenzao wanavyofanya.

KWA TAARIFA YAKO kuna suala la uzinduzi wa video na audio za kwaya mbalimbali nchini ambazo umaarufu wa kuzindua kunaendana na mgeni wa heshima ambaye atachangia kiasi cha fedha ili kuiwezesha kwaya husika kusonga mbele katika mipango ya injili waliyojiwekea. Mwanzoni uzinduzi haukuwa maarufu nchini, kwaya ama waimbaji binafsi walikuwa wakibariki kazi zao makanisani mwao bila matangazo ya kwamba watakuwa na tukio hilo labda upate kusikia kutoka kwa watu wanaosali kanisa ambalo kwaya hiyo wanatoka.

KWA TAARIFA YAKO kwaya iliyofungua kwaya nyingine nchini hususani kwa jijini Dar es salaam kufanya mambo ya uzinduzi na matangazo kuonekana kwenye runinga ni kwaya ya 'Neema
N.G.C wakati wa uzinduzi album mpya hivi karibuni.
Gospel Kwaya' kutoka kanisa la African Inland Church (AIC). Kwaya hii ilizindua video yake ya kwanza iitwayo 'Dunia Imechafuka' mwanzoni mwa miaka ya 2000 na matangazo ya uzinduzi kurushwa kwenye runinga ya ITV (kama GK haijakosea) huku ukumbi ukiwa Diamond Jubilee VIP. Haikuwa ajabu kwa video kwakuwa kwaya kama Ulyankulu Tabora, Tumaini Shangilieni Kwaya Arusha,  na Uinjilisti Sayuni Kinondoni Lutheran walikuwa wameshatoa video zao miaka mwishoni mwa miaka ya 90.

KWA TAARIFA YAKO ninachotaka ukifahamu ni kwamba Neema Gospel Choir (N.G.C) ndio kwaya ya kwanza kufanya uzinduzi mkubwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kutangaza uzinduzi wao kupitia runinga. Baada ya Neema kufanya uzinduzi wao uliofanikiwa sana, kwaya nyingine zikafuata kwa kuanza kutangaza zinduzi zao pamoja na kukodi kumbi za kuzindulia wakati awali ilikuwa wanazindulia makanisani mwao.




KWA TAARIFA YAKO kama haitoshi baada ya kutoa kanda hiyo ya 'Dunia Imechafuka' Neema wakaendelea na huduma na kufanikiwa kutoa video nyingine huku pia ikishuhudiwa kwaya kama Haleluya kutoka Tabata wakitangaza kanda yao 'Unang'ang'ania dhambi itakupeleka pabaya' ikipata umaarufu kwa kuonyeshwa kwenye runinga pamoja na kwaya nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanya uzinduzi. KWA TAARIFA YAKO kama haitoshi Neema iliongeza nguvu kwenye masuala ya muziki miaka takribani sita sasa kwakupata timu ya vijana wanaopiga muziki mzuri kama ilivyoshuhudiwa kwenye video yao ya 'Kuna mamba Kivukoni'. Sasa ni takribani wiki mbili toka kwaya hiyo izindue album yake mpya ya sauti iitwayo 'Haki yake Mungu' moja kati ya album bora za muziki wa injili nchini kwa ujumla. 

KWA TAARIFA YAKO miaka mitatu iliyopita kulikuwa na picha ya sauti (video) ya kundi la Joyous Celebration ya Afrika ya kusini (Joyous 15 part 1) ambayo iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook na mmoja wa wanamuziki wa kwaya hiyo na majadiliano yakaanzia hapo, katika majadiliano hayo wanamuziki hao wakasema inawezekana kabisa kwaya ikapiga viwango vya Joyous hata kuzidi kama watu wataamua kuwa serious, maneno hayo ndiyo nayaona majibu sasa, mwanzo wa sasa wa Neema Gospel ni kweli inataka kuimba viwango vya juu zaidi na kutaka kufahamika kimataifa, ili kujua nazungumzia kitu gani nunua album yao mpya utaamini kwanini nimekujuza.


Timu ya wanamuziki Neema Gospel Choir.